Tanzania KITUKO: DIAMOND AFANYA BETHIDEI KITANDANI



STAA wa wimbo wa Number One, Nasibu Abdul ‘Diamond’ amefanya kituko cha aina yake kwa kufanya sherehe ya bethidei yake kitandani mwanzo mwisho.
Diamond na mchumba wake Penniel Mungilwa ‘Penny’ wakiwa kitandani.
Tukio hilo lililowashangaza wadau walioziona picha za sherehe hiyo lilifanyika juzikati nyumbani kwake Sinza-Mori, jijini Dar, ambapo ilihusisha watu wachache ambao mwenyewe aliwachagua.
Akizungumzia tukio hilo, mmoja wa ndugu wa karibu wa Diamond ambaye hakupenda kulianika jina lake gazetini, alisema walikaa kama ndugu na kuchagua watu wenye umuhimu na kufanya pati hiyo.
“Kiukweli hatukuhitaji wingi wa watu katika sherehe yetu na ndiyo maana unaona wako watu wachache tu ambao ni wa muhimu kwetu,” alisema ndugu huyo wa Diamond.
Chanzo kingine kilicho karibu na Diamond kilipenyeza ‘ubuyu’ kuwa Diamond na mchumba wake Penniel Mungilwa ‘Penny’ waliamua kuifanyia sherehe hiyo kitandani kama ishara ya kuoneshana upendo na kusahau maneno ya watu wasiopenda penzi lao.
“Dogo alifanya vile ili kumuonesha Penny kuwa bado ana mapenzi naye ndiyo maana akaamua sherehe yake ifanyike chumbani kwao wanakolala kila siku,” kilisema chanzo hicho na kuongeza:
“Penny ameonekana kufurahi na kuwapiga vijembe vya waziwazi wale wote waliosema Diamond amerudiana na Wema na kuwaambia walie tu maana yeye ndiye analala naye kitanda kimoja.”

Comments