TANZANIA: WEMA, DIAMOND KURUDIANA... USHAHIDI WAANIKWA


LICHA ya wenyewe kukanusha kwamba hawajarudiana, ushahidi kwamba masupastaa wa Bongo, Nasibu Abdul ‘Diamond’ na Wema Sepetu ni wapenzi tena umeanikwa, Risasi Jumamosi linao.
Kwa sasa Wema yuko nchini China akivinjari, lakini habari zisizo na hata chembe ya shaka, zinasema Diamond naye ametua huko na kuungana na mchumba wake huyo wa zamani.
WAONEKANA MITAANI
Picha za mnato za wawili hao wakiwa kwenye mitaa mbalimbali jijini Beijing, China zimenaswa na kusambazwa kwenye mitandao makini hasa baada ya Diamond hivi karibuni kukanusha kupitia redio moja kwamba hajarudiana na Wema.
Ndani ya picha hizo, Diamond anambusu Wema kila wakati bila kujali macho ya Wachina ambao kwao hawana mapenzi ya hadharani kama wazungu.
WAONEKANA CHUMBANI
Picha nyingine zinawaonesha wawili hao wakiwa chumbani katika mavazi ya kulalia huku wameshika simu kwa ajili ya kujipiga picha, kama kawa Diamond anambusu mlimbwende huyo huku naye akionekana kukolea.
USHAHIDI KWA PENNY
Katika Gazeti la Amani la Oktoba 3, 2013 ukurasa wa mbele kulikuwa na habari yenye kichwa; Habari ya mjini…WEMA,
DIAMOND WARUDIANA!
Miongoni mwa watu walioongea na gazeti hilo kuhusu kurudiana kwa wawili hao ni mchumba wa sasa wa Diamond, Penniel Mungilwa ‘Penny’ ambapo alikiri kusikia Wema na Diamond kurudiana lakini akasema hawezi kukubali hadi aone picha. Picha ndiyo hizo ukurasa wa kwanza. Baadhi ya watu wanaotoa maoni yao mtandaoni, wanamcheka!
ANACHODAI DIAMOND
Kwa upande wake Diamond alipoulizwa na mapaparazi wetu kuhusu kurudiana na Wema na kwamba wapo wote China wakila bata, alikataa akidai yupo Nigeria kikazi zaidi.
Akadokezwa: Kama upo Nigeria mbona kuna picha unaonekana umepiga ukiwa na Wema?
Akashtuka: He! Hebu n’tumie picha moja niione.
Alipotumiwa picha moja akacheka kidogo kisha akasema: Hii ni filamu bwana. Mimi sijarudiana na huyo demu (Wema).
KUMBUKUMBU MUHIMU
Baada ya kuachana siku za nyuma, Wema na Diamond waliwahi kudaiwa kwamba wamerudiana na wakahojiwa katika kipindi cha You Heard cha Redio Clouds FM ambapo wote walikanusha kurudiana. Halafu Wema akaulizwa: Lakini si bado unampenda Diamond?
Majibu yake: Siwezi kumpenda Diamond wewe.
MASWALI YA MSINGI
Diamond aliwahi kumrekodi Wema akijibembeleza kwake warudiane, akaipeleka sauti hiyo redioni na ikasikilizwa na raia. Kwa Wema ule ulikuwa udhalishwaji mkubwa. Je, ni kweli anaweza kumkubalia msanii huyo washuti filamu pamoja?
Diamond anajua Penny ameambiwa wao wamerudiana, alipoulizwa na Penny alimjibu achana na maneno ya watu. Je, Penny anaweza kumruhusu Diamond acheze filamu na Wema?
Kama ni filamu, Diamond hana vifaa vya kushutia wala kampuni ya filamu, Wema ana kampuni kubwa yenye vifaa vyote, kwanini ‘makamera-mani’ wake wote wabaki Dar, huko China wamekodi vifaa? Na kameramani je, pia wamemkodi? Haiingii akilini.
UKWELI UTABAKI PALEPALE
Katika yote, ukweli unabaki palepale kwamba, wawili hao kwa sasa ni mapenzi motomoto. Chanzo kimoja cha karibu yao huko China kimeliambia Risasi Jumamosi kwamba, wawili hao wanatanua kama wako fungate, tena wanalala na kuamka!

Comments

Popular Posts